IGP Sirro Awataka Wananchi Msidanganywe Kuhusu Chanjo Ya Corona


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewataka Wananchi na Watanzania kwa ujumla wasidanganywe na watu wa chache au kikundi cha watu wanaowahamasisha kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kuto kuchanjwa chanjo ya Uviko-19 ambapo zoezi la uchanjwaji wa chanjo hiyo lilizinduliwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es salaam.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati wakiandikishiana hati ya makubaliano kati ya Shirika la Bima la Taifa na Jeshi la Polisi kupitia Shirika lake la Uzalishajimali ambapo shirika hilo litaweza kuwa wakala wa bima za maisha na ajali kwa watendaji wa Jeshi hilo la Polisi pamoja na familia zao huku Jeshi hilo likitoa ahadi ya kutanua wigo ili bima hiyo ya maisha iweze kuwafikia hata waendesha pikipiki maarufu bodaboda.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa Dkt. Elirehema Joshua amesema kuwa licha ya kuwepo kwa idadi ndogo ya wananchi wenye ufahamu wa masuala ya bima za maisha, ajali na mali ambapo kupitia shirika la uzalishajimali la Jeshi la Polisi litakuwa na wigo mpana wa kuwafikia wananchi pamoja na kuwezesha Watanzania wote kupata elimu na huduma zote za bima zinazopatikana nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments