CHUO KIKUU IRINGA CHAJIPANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA KAZI




Chuo Kikuu cha Iringa (UOI) kimewakaribisha wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kujiunga na mwaka wa masomo wa 2021/22 kwani watafaidika na kozi mbalimbali ikiwemo ya Shahada ya Masoko na Ujasiriamali itakayowasaidia kukabiliana na tatizo la ajira kwa kuanzisha kampuni zao baada ya kuhitimu masomo yao chuoni hapo.

Hayo yamesemwa na Mhadhiri wa Chuo hicho Angel Ezekiel katika Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini(TCU) yanayondelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo wamejipanga kufundisha kozi kwa nadharia na vitendo ili kutengeneza kundi kubwa la wahitimu wanaoweza kulimudu tatizo la ajira hapa nchini kwani wataweza kuanzisha kampuni zao wenyewe.

"Tunachanganya nadharia na vitendo kuendana na soko la ajira wanafunzi watakaojiunga nasi watamaliza masomo yao wakiwa wanaweza kujiajiri Barani Afrika ndio chuo kipekee  kinachofundisha kwa vitendo masuala ya biashara na ujasiriamali", amesema Angel.

Amebainisha kuwa kupitia shahada hiyo wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo watapata fursa ya kufundishwa jinsi ya kuanzisha biashara chini ya usimamizi wa walimu waliobobea hivyo mara watakapohitimu wataendelea nazo.

Ameongeza kuwa wanafunzi watakaosoma taaluma ya Uhandishi wa Habari watafundishwa katika mazingira ya nadharia na vitendo katika matukio yanayofanyika uoi kwani chuoni hapo kuna radio ya Hope Fm, Gazeti la chuo pamoja na Tv.  

Amesisitiza kuwa chuo hicho kinafundisha kozi mbalimbali katika ngazi ya Cheti, Astashahada, Shahada na Shahada ikiwemo Uhandishi wa Habari, Sheria, Mendeleo ya Jamii, Usimamizi wa Biashara, Ualimu, Utawala, Masoko, Utafiti, Manunuzi, Utalii, Kompyuta pamoja na uchungaji.

Maonesho hayo yalizinduliwa Julai 27 mwaka huu katika viwanja hivyo na Baraza la Mapinduzi na Kiongozi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Mhandisi, Zena Ahmed Said na yanatarajiwa kufikia tamati Julai 31, 2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments