IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO KWA MAKAMANDA WA POLISI..MULIRO APELEKWA DAR


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro
***
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi, ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

Katika mabadiliko hayo, .Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya amehamishwa kutoka kuwa Kaimu Kamishna wa Fedha na Logistiki Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani nchini na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kipolisi Rufiji, – Onesmo Lyanga amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamanda Gilles Muroto ambaye anastaafu.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ramadhan Ngh’anzi amehamishwa kutoka kuwa Boharia Mkuu kwenda kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, huku Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mwamini Rwantale akihamishwa kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambako alikuwa Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.

IGP Sirro pia amemhamisha Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, – Muliro Jumanne kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Kamishna wa Polisi Camillius Wambura.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Zuberi Chembera, yeye amehamishwa kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa jinai Zanzibar kuchukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Hamad Khamis Hamad.

Naye Kamishna Msaidizi wa Polisi Stella Richard amehamishwa kutoka kuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم