BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU (HESLB) YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA POTOFU INAYOSAMBAZWA MITANDAONI
الاثنين, أكتوبر 19, 2020
Na Mwandishi Wetu, HESLB
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefafanua kuhusu taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na utaratibu wa kupata majibu ya maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2020/2021.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu (Oktoba 19, 2020) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema HESLB bado haijatoa orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo na kuwa kwa sasa, kazi ya uchambuzi wa maombi ya mkopo yaliyowasilishwa inaendelea.
Badru amesema taarifa hizo zisizo sahihi zinazosambaa mitandaoni zinawaelekeza waombaji mikopo kupakua mfumo (application) katika simu zao utakaowawezesha kuona orodha ya wanafunzi waliopangiwa mkopo kwa mwaka 2020/2021.
“Taarifa rasmi kuhusu HESLB, zikiwemo zinazohusu wanafunzi wanaopangiwa mkopo zitatolewa kuanzia Novemba 10, 2020 kupitia akaunti walizotumia kuomba mkopo inayofahamika kama SIPA – Student’s Individual Permanent Account,’’ amesema Badru katika taarifa yake.
Badru ameongeza kuwa taarifa kuhusu wanafunzi waliopangiwa mikopo pia zitatolewa kupitia vyombo vya habari, tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) na mitandao ya kijamii ya HESLB ambayo ni twitter, instagram na facebook kwa jina la ‘HESLB Tanzania’.
Serikali imetenga kiasi cha Tsh Bilioni 464 katika mwaka wa masomo 2020/2021, zinazotarajia kusomesha jumla ya wanafunzi 145,000 wakiwemo wanafunzi 54,000 wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 91,000 wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.
MWISHO
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin