BENKI YA I&M YASHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam huku wakiwa wameshikilia madafu mikononi
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam huku wakinywa maji ya dafu kama wanavyoonekana 
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa kwenye jamvi na wengine wamesimama 
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakikata keki ikiwa ni ishara ya wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

BENKI ya I&M Tanzania imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwa kutambua mchango muhimu unaotolewa na fanyakazi wake katika kuwahudumia wateja wao kwa viwango vya juu na kuhakikisha kuwa wanakuwa wenye furaha wakati wote.
 
Hafla hiyo ilifanyika maktaba square  jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya benki hiyo, ikiambatana na shughuli mbalimbali kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa wateja wanaothaminiwa na pia wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu muhimu la kutoa huduma bora kwa wateja wakati wote.
 
Miongoni mwa shughuli za kusherehesha hafla hiyo na wiki ya huduma kwa wateja zilizofanywa na benki hiyo ni pamoja na Maofisa wa juu na waandamizi wa benki hiyo akiwamo Afisa Mtendaji  Mkuu, walichukua jukumu la kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali kwa siku ya jana.
 
Sheherehe hiyo ya wiki nzima ni matokeo ya kujitolea kwa benki hiyo ya I&M katika kuongeza ushiriki wa wafanyakazi katika kuunga mkono kaulimbiu ya mwaka huu ya siku hiyo inayosema kuwa, ‘Timu ya ndoto’.
 
Mbali na ushiriki wa watendaji wakuu, maafisa waandamizi katika kufanya jukumu la huduma kwa wateja, pia wafanyakazi wote wa benki hiyo walipokea barua binafsi za shukurani kwa bidii yao na kujitolea kwao katika kuleta matokeo chanya na furaha kwa wateja katika benki hiyo.
 
Mkuu wa Mauzo ya rejareja wa benki hiyo, Lilian Mtali alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wanataka onyesha thamani ya watoa huduma kwa wateja.
 
“Sisi benki ya I&M tunataka kutumia wiki hii ya huduma kwa wateja kuhakikisha kuwa tunawaonyesha thamani na ukarimu wateja wetu,lakini pia kuunga mkono na kutambua kazi nzuri na kubwa inayofanywa na maafisa wa huduma kwa wateja kama dawati namba moja ambalo ni nembo na kilelezo cha huduma bora za benki.
 
“Kwani sote tunatambua kuwa dawati la huduma kwa wateja ndilo limebeba sura na kilelezo cha huduma bora zinazotolewa na benki, wamekuwa wakaifanyakazi kwa bidi kwani hata pale wateja wanapokuwa na jazba, wao wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kuwa wanakamilisha mahitaji yao na kuwaacha wakiwa na furaha jambo ambalo ni kipaumbele cha benki,” alisema Lilian.
 
Wiki ya Huduma kwa Wateja ni maadhimisho ya umuhimu wa huduma kwa wateja na ya watu ambao wanahudumia na kusaidia wateja kila siku. 
 
Hafla hiyo huadhimishwa kila mwaka wakati wa wiki ya kwanza ya Oktoba na wafanyabiashara wote na mashirika yanayolenga huduma kote ulimwenguni, ambayo hutambua umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wateja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم