KAMATI YA TAIFA YA USALAMA BARABARANI KWA WATU WENYE ULEMAVU YATOA MAFUNZO

 

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu akifungua mafunzo ya alama sita mpya za usalama barabarani kwa makundi maalumu kushoto wa kwanza mwenye shati jeupe  ni Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa akifuatiwa na Mwenyekiti wa (NCPDRS) Jutoram Kabatele kulia ni Katibu Mkuu wa (NCPDRS) Hamisi Cheni
Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa (NCPDRS) Jutoram Kabatele kushoto akisistiza jambo wakati wa mafunzo hayo kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu na Katibu Mkuu wa (NCPDRS)  Hamisi Cheni
Mwenyekiti wa RSA mkoa wa Tanga Eddo Mwakimwagile akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Tanga na washiriki kushoto ni Mwenyekiti wa (NCPDRS) Jutoram Kabatele na kulia ni Katibu Mkuu wa NCPDRS Hamisi Cheni
KAMATI ya Taifa ya Usalama Barabarani kwa watu wenye ulemavu imetoa mafunzo ya alama sita mpya za usalama barabarani katika makundi maalumu mkoani Tanga ambazo zitakuwa mkombozi kwao.

Mafunzo hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini Tanga na kufunguliwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mratibu wa Mradi wa alama sita mpya maalumu za usalama barabarani kwa watu wenye ulemavu (NCPDRS) mikoa ya Tanga na Mtwara Christopher Mbelwa alisema msimamizi wa uwepo wa alama sita mpya za makundi maalumu.

Alisema mpango huo wa mradi wa utoaji wa elimu na alama mpya sita umefadhiliwa na Foundation for Civil Society (FCS) tokea mwaka 2010 kwa kuanzia mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar  na mwaka huu 2020 wamepata ufadhili kwa mikoaya Tanga na Mtwara.

Mratibu huyo alisema matarajio ya taasisi yao ni kutoa elimu hiyo nchi nzima lakini kwa kuendesha mradi huo ni gharama kubwa hivyo wanapenda kutoa shukrani kwa Foundation for Civil Society (FCS) huku wakijitahidi kutafuta wafadhili wengine.

“Wafadhili hao utakaotafuta watasaidiana na  Foundation for Civil Society kuhakikisha mradi huu unakamilika ifikapo mwaka 2022 lakini pia tunatoa Pongeza zetu kwa utekelezaji wa uwekaji barabarani alama hizi kwani tokea tumeingia mkoa wa Tanga tumeziona”Alisema

Pamoja na kutoka elimu kwa madereva walengwa, makundi maalumu na jamii kwa ujumla ili wazitambue alama hizo ambazo ni muhimu kwao kuweza kuzifuata.

Alisema usafiri salama katika vyombo vya umma akitolea mfano miundombinu ya mabasi, meli,treni na ndege ili kumfanya mtu mwenye ulemavu wa viungo aweze kupanda na kushuka kwa urahisi.

Aidha alisema pia uwepo wa mafunzo ya udereva kwa walio wenye ulemavu ili waweze kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ambapo hiyo ni utekelezaji wa sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004.

Awali akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga RTO SP Leonard Fungu alisema kwamba vyombo vya kusimamia sheria visipo simama imara madereva wakorofi wataendelea kusababisha ajali.

“Hivyo ni lazima tuhakikisha tunakuwa makini zaidi lakini niwapongeze askari wa usalama barabarani mkoa wa Tanga wamekuwa wakisimama imara zaidi katika kusimamia ipasavyo sheria za usalama”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba mafunzo hayo ni muhimu kwani yatawapa uelewa jamii hiyo na kuweza kuepukana na ajali ambazo wanaweza kukumbana nazo wanapokuwa wakitumia barabara hizo.

“Lakini nisema RSA ni jicho la tatu la usalama barabarani kwani wamekuwa mstari wa mbelea kutoa taarifa pindi wanapobaini uwepo wa vitendo visivyosahihi barabarani vinavyofanywa na madereva”Alisema

 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments