TANESCO YAKUTANA NA WACHIMBAJI MADINI, WAMILIKI MASHINE KUTOA ELIMU YA USALAMA NA MATUMIZI BORA YA UMEME




Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo, pamoja na wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka Salawe na Solwa, wilayani Shinyanga wameaswa kuacha kununua vifaa cha kusukuma mashine na Makarasha ya kusagia mawe yenye dhahabu (Motor) zenye uwezo mdogo, ambazo zinawasababishia matumizi makubwa ya umeme.

Zoezi la utoaji elimu hiyo limefanyika kwa muda wa siku mbili, kwa lengo la kutoa elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme, ili kuwaepusha na gharama zisizo za lazima kwa mtumiaji.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu hiyo Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, amesema wametoa elimu kwa wamiliki hao wa mashine na wachimbaji wadogo wa madini, ili kuhakikisha usalama wa umeme na matumizi bora ya nishati katika kazi zao za uzalishaji.

"Tumekuja kutoa elimu kwenu ya usalama wa umeme na matumizi bora ya nishati, mara baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwenu kuwa mnatumia gharama kubwa za umeme, ambapo tumegundua motor mnazotumia zina uwezo mdogo, na hivyo kusababisha matumizi makubwa ya umeme," amesema Bigirwamungu.

"Mbinu ambayo ninawapa ili kukwepa matumizi makubwa ya umeme, ni kuacha kununua motor zenye uwezo mdogo, pamoja na kuacha kuzifanyia matengenezo zaidi ya mara mbili, bali mnunue mpya tena zenye ubora zaidi bila ya kujali bei na siyo kununua feki," ameongeza.

Naye meneja masoko Monica Masawe kutoka Shirika hilo la umeme Tanesco Makao makuu, alitoa wito kwao kuacha kufunga mfumo wa umeme (Wiring) kwa kutumia mafundi wa mitaani, ambao siyo wataalam na wanaweza kusababisha jengo kuungua moto.

Kwa upande wake Afisa mahusiano na huduma kwa wateja Tanesco Mkoani Shinyanga Sara Libogoma, amewataka wateja hao pale wanapopatwa na changamoto za umeme, wawasiliane na Shirika hilo mapema iwezekanavyo kupitia ofisi ndogo zilizopo karibu na maeneo yao, ili wapatiwe ufumbuzi wa haraka.

Nao baadhi ya wateja hao wa Tanesco walishukuru kwa elimu hiyo na kuomba iendelee kutolewa mara kwa mara ili waepukane na matumizi yasiyo ya lazima ya kuongeza gharama za umeme, hali ambayo itaongeza pato lao binafsi na taifa kwa ujumla.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI



Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo. Picha zote na Marco Maduhu

Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka Salawe.

Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka Solwa.

Meneja masoko Monica Masawe kutoka Shirika la umeme Tanzania Tanesco Makao makuu, akitoa elimu ya usalama katika matumizi ya umeme kwa wachimbaji wadogo wa madini Mwakitolyo eneo la Nyaligongo namba 2.

Meneja masoko Monica Masawe kutoka Shirika la umeme Tanzania Tanesco Makao makuu, akitoa elimu ya usalama katika matumizi ya umeme kwa wachimbaji wadogo wa madini Mwakitolyo eneo la Nyaligongo namba1.

Meneja masoko Monica Masawe kutoka Shirika la umeme Tanzania Tanesco Makao makuu akitoa elimu kwa wamiliki wa mshine za kusaga na kukoboa nafaka- Salawe juu ya gharama za umeme.

Afisa mahusiano na huduma kwa wateja Tanesco Mkoani Shinyanga Sara Libogoma, akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo, na kuwataka pale penye changamoto za umeme watoe taarifa kwa Shirika hilo kupitia ofisi ndogo zilizopo maeneo yao.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.

Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.

Wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka kutoka Salawe, wakiwa na maofisa wa Tanesco katika utoaji elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme.

Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, (kulia), akitoa maelekezo kwa mmiliki wa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka Richard Machibya (katikati) juu ya kununua Motor zenye uwezo mzuri ambazo zitasukuma mashine na kuondokana na matumuzi makubwa ya umeme.

Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, akitazama Motor ya kusukuma mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.

Muonekano wa Motor ambazo zinatumika kusukuma mashine.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم