CHADEMA WATOA TAMKO TUNDU LISSU KUVULIWA UBUNGE


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimedai kuwa hatua ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuvuliwa Ubunge na kuzuiliwa kugombea Ubunge kwa miaka 5 inalenga kumzuia kutowania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020.


Kauli hiyo ya CHADEMA imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha hicho, DR Vincent Mashinji wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya maamuzi ya Spika kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kushindwa kuhudhuria Bungeni.

"Kuna ibara inamfunga Lissu kugombea ndani ya miaka mitano, na inambana hawezi kugombea Urais wa Tanzania kama hana sifa za kugombea Ubunge Tanzania, naomba tutafakari tukiwa tumebakiza mwaka mmoja kwenda Uchaguzi Mkuu 2020", amesema Mashinji.

"Muda wote ambao Spika anadai Lissu hajui alipo, Bunge limekuwa likimlipa mshahara, hili jambo si la kawaida, na watanzania wote wanajua Mama Samia Suluhu alikwenda kumsalimia Lissu Nairobi, na alienda kumpatia salamu za pole kutoka kwa Rais.", ameongeza Mashinji.

Mapema Ijumaa ya wiki iliyopita, Spika Job Ndugai alitangaza kumvua Ubunge Tundu Lissu kwa kile alichokidai kiongozi huyo kuwa na mahudhurio hafifu ndani ya Bunge.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527