ACHAPWA VIBOKO 40 KISA KULA EMBE OVYO OVYO HADHARANI MWEZI WA RAMADHAN

 Ibrahim Ismail, jamaa mwenye umri wa miaka 20 amepatikana na hatia ya kula embe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na kupokea mijeledi 40 kwa kosa hilo.

 Ismail ambaye alituhumiwa kula wakati Waislamu wengine wakifunga, amepatikana na hatia hiyo na mahakama inayoongozwa na sheria za Shariah katika eneo la Ringim, mjini Jigawa, nchini Nigeria. 

Ibrahim Ismail alipokea mijeledi 40 kwa kula embe wakati wa mfungo wa Ramadhan   katika soko la Ringim baada ya afisa wa mahakama kumsomea mashtaka

Jaji Safiyanu Ya’u, alitoa amri kwamba jamaa huyo acharazwe mijeledi 40 hadharani ili iwe funzo kwake na kwa wengine ambao walikaidi sheria za mwezi mtukufu. 

Kushiriki mlo kwa wakati usiofaa inakinzana na sheria za kifungu cha 370 za mji wa Jigawa, Nigeria. 

 Awali, Nabahani Usman ambaye ni kamanda wa polisi wa Kano Hisbah, alionya kwamba yeyote atakayepatikana akila ovyo ovyo hadharani atachukuliwa hatua kali kwa kukaidi sheria za mfungo wa Ramadhan. 

Aliongeza kuwa, wale watakaonaswa wataachiliwa huru iwapo watatoa ushahidi wa ripoti ya daktari kwamba walikuwa wanaruhusiwa kula kwa sababu za kiafya. 
Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527