Angalia Picha : TAMASHA LA KUABUDU NYOKA



Kila mwaka katika kijiji cha Cocullo huko Italia, sanamu ya mtakatifu inayozungukwa na nyoka walio hai huzungushwa mitaani.

Tamasha hilo ambalo hufanyika kila Mei mosi kila mwaka katika sanamu ya mtakatifu San Domenico di Sora ,

Tamasha hilo lilianza kuadhimishwa tangu karne ya kumi na moja wakati ambapo nyoka waliondolewa kutoka kwa wakulima kwa namna ya kushangaza .

Hata hivyo , asili ya tamaduni hiyo ilianza kuabudiwa huko katikati mwa mji wa Angitia, na ilifahamika kama nyoka wa miungu wa Roman.
Watu wengine huwa wanavaa mavazi ya asili ya watu wa mji wa Abruzzo.
Wakamataji nyoka huwa wanawakamata nyoka aina nne ambao hawadhuru na kuwakabidhi kwa watu wanaoabudu nyoka hao.
Na taratibu, nyoka hao huwa wanawekwa kwenye sanamu ya mbao ya San Domenico .
Nyoka wengine wengi huwa wanaongezwa hadi sanamu ya San Domenico ikiwa imefunikwa kabisa nyoka.
Baada ya sanamu huyo kuvishwa nyoka mwili mzima, hubebwa na kuzungushwa barabarani ikiwa ndio utaratibu wa
Wakati wengi huwa wanaambatana na sanamu hiyo, wengine huwa wanaangalia kwa pembeni.
Baada ya tamasha hilo kumalizika, nyoka huwa wanaachiwa kurudi porini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527