MUFTI WA TANZANIA ASHIRIKI FUTARI ILIYOANDALIWA NA KIBADA GARDENS KIGAMBONI,ATOA NENO KWA WAGENI WAALIKWA


Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wageni wakibadilishana mawazo kabla ya kufuturu.
Muda wa Kufuturu (Iftar)
Maulid Kitenge (MC) akifurahia jambo pamoja na Mufti, Sheikh Abubakar Zubeir.
Mufti akitoa mawaidha kwa watu mbalimbali waliofika Kibada Gardens kwa ajili ya Iftar maalum iliyoandaliwa siku hiyo,Mufti amewataka Waislamu waendelee kumcha Mungu na kuendelea kufanya matendo mema yanayompendeza Mwenyezi Mungu,na kwa si kwa wakati huu tu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani,lakini pia wakati wote.
Sheikh wa msikiti wa Kibada akikabidhiwa baadhi ya vitu kwa ajili ya Futari kwa wakazi wa Kibada.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mr. Ali Davutoglu akipeana mkono na Sheikh wa wilaya ya Kigamboni, Mr. Sharrif Hassan wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Kibada Gardens Dar es Salaam. Pili kushoto ni Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir bin Ally
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir bin Ally akitoa maneno ya hekima kwa baadhi ya watu waliofika katika Iftar maalum iliyoandaliwa na Kibada Gardens, Kigamboni Dar es salaam.
Mufti wa Tanzania pamoja na baadhi ya masheikh wa bakwata wakiwasili Kibada Gardens kwa ajili ya Iftar iliyoandaliwa maalum katika mfungo wa Ramadhan unaoendelea.
 Kibada Gardens imeandaa Iftar maalum ambayo ilihudhuriwa na Mh. Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir Bin Ally na Mh. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم