WADAU WAANZA KUJITOKEZA KUMSAIDIA BINTI ANAYETESEKA NA UGONJWA WA NGOZIWadau wa michezo wa mazoezi (GYMNASTICS) Kutoka Bwalo la Polisi Shinyanga Mjini wamejitokeza kumchangia fedha za matibabu mama Happiness Stephen mkazi wa mtaa wa Busulwa kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga ambaye anauguliwa na mtoto wake Aitwaye Rogathe Cyprian Makala ambaye anasumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.

Akizungumza leo Mei 31, 2019 Katibu wa kikundi hicho cha mazoezi Paulina Dario wakati akimkabidhi msaada wa fedha za matibabu mama huyo pamoja na mtoto wake shilingi 230,000/-, amesema wameguswa na tatizo analosumbuliwa mtoto huyo, ambapo taarifa zake waliziona kupitia Mtandao wa Malunde1 blog ndipo wakaona ni jambo njema kuchangishana na kupatia msaada huo.


Amesema wao kama wadau wa michezo ya mazoezi GYM, baada ya kuona taarifa hizo ndipo wakaona ni vyema wakajitokeza kumsaidia mama huyo ili kutoa hamasa kwa watu wengine, zikiwemo na taasisi binafsi waguswe na tatizo ambalo anakabiliwa mtoto huyo ili aweze kupata matibabu na kisha kuendelea na masomo yake .


“Tunatoa wito kwa wadau wengine, zikiwemo na taasisi binafsi waguswe na tatizo hili ambalo anakabiliwa mwana Shinyanga mwezetu, ambapo ni bora sisi tukawa mfano wa kuigwa kwa kutoa kile tulichonacho, kuliko kuja kusaidiwa na watu kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga litakuwa ni jambo la aibu sana,”amesema Dario.


Kwa upande wake mama huyo Happines Stephen, ametoa shukrani kwa wadau ambao wamejitokeza kumsaidia fedha hizo za matibabu za mtoto wake, vikiwamo na vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii Blogs, na kubaninisha kuwa Mungu atawalipa.


Kiasi cha Shilingi Milioni 4,536,000 zinahitajika kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake huyo, ambapo kila mwezi anatakiwa kulipia dawa za matibabu kutoka India Shilingi 504,000 kama dozi ambayo itatumiwa ndani ya miezi tisa ndipo atapona tatizo lake hilo la ugonjwa wa ngozi.


Inaelezwa kuwa  homoni za binti huyo zipo kwenye njia ya mkojo, na asipopata matibabu ya haraka ugonjwa huo utageuka na kuwa kansa na ataweza pia kuwa anazaa watoto wenye kisukari, na kichwa kikubwa na hata kuambukiza watu wengine kwa njia ya kuchangia choo.


Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:


Vodacom : 0764206669 - Happines Makala

Halotel: 0626845953 Eliud Makala

Soma hapa>>BINTI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI MSAADA WAKOWadau wa michezo wa mazoezi (GYMNASTICS) Kutoka Bwalo la Polisi Shinyanga Mjini wakikabidhi msaada wa fedha Shilingi 230,000/- kwa ajili ya matibabu ya binti
Rogathe Cycprian ambaye anasumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi wa kwanza kushoto ni Mhasibu wa GYM hiyo Rhobi Wambura akifuatiwa na mama wa mtoto na Rogathe, na wa kwanza mkono wa kulia ni katibu wa GYM hiyo Paulina Dario wakikabidhi msaada wa fedha baada ya kumaliza kufanya mazoezi leo majira ya saa mbili usiku.

Binti Rogathe Cycprian akionyesha jinsi ugonjwa huo wa ngozi ambao unamtesa kwa kutokwa na upele mwili mzima ,ambapo ikifika muda wa usiku huwa halali ana kesha na ajikuna mpaka asubuhi.

Muonekano wa upele jinsi unavyomsumbua binti huyo.

Wadau wa michezo wa mazoezi (GYMNASTICS) Kutoka Bwalo la Polisi Shinyanga wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kukabidhi msaada wa fedha za matibabu baada kumaliza kufanya mazoezi leo saa mbili usiku.

Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم