WAITARA : VIONGOZI JENGANENI MAHUSIANO MAZURI NA WAANDISHI WA HABARI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amewataka viongozi kutoka ngazi mbalimbali  kujenga Mahusiano Mazuri na waandishi wa habari kwani ndio nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Waitara amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa elimu   katika kikao  cha Maandalizi ya Mashindano ya Umoja wa Michezo  shule za Sekondari ,Tanzania [UMISETA] unaodhaminiwa na Coca cola.

Mhe.Waitara amesema waandishi wa habari wanatakiwa kupewa kipaumbele katika mambo  ya  Msingi ya Serikali vivyo hivyo katika mashindano hayo ya UMISETA ni vyema vyombo vya habari vikatumika kuibua vipaji vya wachezaji mbalimbali na serikali za mitaa  kuwawezesha wanahabari katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nguzo muhimu.

“Sio kwamba mpaka aje Mkurugenzi,Waziri  No.hata wewe unaweza ,mwanafunzi kafanya vizuri tangaza hiyo,shule za kata zinatoa matokeo mazuri tangaza hiyo.Kuna Ofisi zingine zina pwaya  ni mzigo  akimwona mwanahabari hata  ushirikiano hatoi yeye yupoyupo tu.

"Hivyo katika Mashindano haya tumieni vyombo vya habari,kupitia blogs,redio,magazeti ,vyombo vya habari vyote kuhamasisha michezo.”

Aidha waitara ameagiza Maafisa elimu wilaya ni mikoa kufuatilia somo la michezo kufundishwa kwa nadharia na vitendo,viwanja vya michezo kufufuliwa,kusimamia makusanyo ya fedha za michezo  na nyimbo za uzalendo ikiwa ni pamoja na wimbo wa Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki kuimbwa hasa kwenye mashindano hayo.

“Unakuta mtu mzima na ofisi yake ukimwambia imba anasingizia ana kikohozi ,tatizo  sio kikohozi bali haujui huo wimbo.hivyo tuhamasishe nyimbo za uzalendo kwa Taifa Letu.”

Katika kuboresha na Kutunza Mazingira Mhe.Waitara ameagiza kila mwalimu apande mti  mmoja wake shuleni na kila mwanafunzi miti miwili nyumbani na shuleni.

Mkurugenzi Idara ya Elimu Tanzania,Julius Nestory amesema watashirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza vipaji vya wanafunzi shuleni huku akipongoza Copa  Coca Cola kwa  kudhamini Mashindano ya UMISETA.

Kwa Upande wake ,Mkurugenzi wa Mambo ya Umma na Mawasilino ,Coca Cola  Haji Mzee Ally amezitaja mikoa atakayoanza katika kuzindua Mashindano ya UMISETA 2019 ni Tabora,Manyara na Ruvuma huku akisema kuwa kutakuwa na mkakati kabambe wa kuzipa zawadi shule zitakazokusanya  takataka  za plastiki  za kampuni yoyote katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira .

Mwenyeji wa Mashindano UMISETA 2019 ni Mkoa wa Mtwara na yanatarajia kuanza mwezi ujao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم