RADI YABOMOA NYUMBA NA KUUA MTU RUKWA


Mtu mmoja mkazi wa kijiji na kata ya Mkoe wilaya ya  Kalambo mkoani Rukwa Girubat Lungwa (34) amefariki dunia baada ya radi kubomoa ukuta wa nyumba yake kisha kuingia ndani na kusabisha kifo chake hapo hapo. 


Tukio hilo la kusikitisha limetokea kufuatia mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha maeneo hayo kisha kusababisha kifo cha mtu huyo moja na mmoja kujeruhiwa wote ndugu wa familia moja. 

Awali akisimulia mkasa huo mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Machipa amesema radi hiyo iliingia ndani ya nyumba ya mwananchi wake kupitia kona ya nyumba yake ambapo kabla ya kuingia ilichoma mifugo yake wakiwemo mbuzi watatu ,kuku na mbwa mmoja. 

Revocatus Lungwa ambaye ni mmoja wa wathirika wa tukio hilo, amesema radi hiyo ilimpiga mara baada ya kusabisha maafa kwa kaka yake. 

Kaimu mtendaji wa kata hiyo Noel Kaduma amekiri kutokea kwa tukio hilo nakusema tukio ni la pili kutokea katika maeneo hayo. 
Peter Kapola- Rukwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم