HALI YA USALAMA MASHAKANI KAMPENI ZA KUMRITHI RAIS KABILA

Kampeni za uchaguzi wa urais zinaanza leo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huku kukiwa na mpasuko mkubwa kwenye upande wa upinzani na hofu juu ya usalama.

Mwisho wa wiki iliyopita wafuasi watatu wa chama tawala cha rais Joseph Kabila wanaripotiwa kuchinjwa katika jimbo la Kasai walipokuwa wakifanya kampeni.

Kura ya kumchagua mrithi wa Kabila aliyekaa madarakani kwa mika 17 itafanyika tarehe 23 ya mwezi ujao, Desemba 2018.

Wiki iliyopita Martin Fayulu alichaguliwa kusimama kama mgombea kinara wa upinzani na ameungwa mkono na wapinzani wengine wenye ufuasi mkubwa kama Moise Katumbi na Jean Pierre Bemba.

Hata hivyo, chama cha upinzani chenye wafuasi wengi zaidi nchini humo cha Union for Democracy and Social Progress tayari kimejitenga na mgombea huyo. Chama hicho kinaongozwa na Felix Tshisekedi kimekuwa mstari wa mbele dhidi ya utawala wa kabila.Haki miliki ya pichaAFPImage captionMartin Fayulu (kati) alichaguliwa kusimama kama mgombea kinara wa upinzani lakini tayari wapo waliojitokeza kumpinga

Siasa za DRC zimekuwa zikitawaliwa kwa mkono wa chuma na Kabila ambaye chini yake vyombo vya usalama vilitumika kuudhibiti upinzani kwa nguvu kubwa.

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limeonya kuwa kunauwezekano mkubwa wa uchaguzi huo kukumbwa na vurugu kutokana na chuki zilizokuwepo za kisiasa na uhasama baina ya raia na vyombo vya usalama.

Chanzo: BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527