TRA YAGAWA MAKONTENA YA MAKONDA KIMYA KIMYAMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeyagawa ‘kimya kimya’ makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yaliyokuwa yakishikiliwa na mamlaka hiyo.

Septemba 5, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo, Richard Kayombo alieleza kuwa iwapo uamuzi wa kuyagawa makontena hayo utafanyika, taasisi zitakazogawiwa zitajulikana.

Hata hivyo, wakati ikisubiriwa kujulikana kwa taasisi hizo, Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere amesema tayari makontena yamekwishagawiwa.

Makontena hayo ambayo yalikosa wanunuzi katika minada yote mitatu iliyoendeshwa na kampuni ya udalali ya Yono yalikuwa na samani za viti, meza na mbao za kuandikia yakidaiwa kodi inayokadiriwa kufikia Sh1.2 bilioni.

Via>>Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم