WANAKIJIJI WAZIKA KIPANDE CHA UTUMBO WA MTOTO ALIYELIWA NA FISI MWANZA


Mabaki ya mguu mmoja na kipande kidogo cha utumbo wa anayeaminika kuwa mtoto wa miaka sita mkazi wa Mwaniko wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Martha Saimon, aliyeliwa na fisi yamezikwa leo kijiji hapo.

Martha, mwanafunzi huyo wa chekechea wa Shule ya Msingi Mwaniko alikutwa na janga hilo alipokuwa amekwenda kujisaidia akiwa na ndugu zake wawili baada ya kumaliza kula chakula cha usiku, Aprili 25.

Bibi wa marehemu Kweji Samwel (52), amesema wamefanya maziko ya mguu mmoja na kipande cha utumbo vilivyopatikana baada ya msako mkali kuutafuta mwili na fisi huyo.


“Taratibu zote za maziko zimefanyika kama kawaida licha ya kuwa tumezika baadhi ya viungo vyake tulivyopata. Jambo hili limetuumiza kwa kiasi kikubwa,” amesema Kweji.


Mwenyekiti wa kijiji hicho, Hezron Lutonja amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji hicho ilikaa na kujadili tukio hilo la aina yake ambalo halijawahi kutokea kijijini hapo.


Amesema kamati hiyo imependekeza kuwaita wawindaji wa kijadi wa wanyama hatarishi (Wama) kutoka Kijiji cha Sumbugu wilaya hapo kwa ajili ya kuwawinda wanyama hao ili wasilete athari zaidi.
Na Twalad Salum, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527