TIGO WAZINDUA KAMPENI MPYA YA TUMEKUSOMA


Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, David Umoh, pamoja na Mtaalam wa Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Biashara, Sarah Cyprian wakizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya Tumekusoma inayoendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma *147*00#. Namba *147*00# itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi, pamoja na kupata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hiyo mpya.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandhishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam.

***
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo imezindua rasmi kampeni mpya ya Tumekusoma, ambayo ni mkakati mkubwa wa kufikia wateja wake na bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda muafaka.

 Kampeni hii ya Tumekusoma pia inaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00# itakayowawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi.

 Wateja wa Tigo watakaotumia namba hiyo mpya pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hii mpya.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya Tumekusoma jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alisema, ‘Tumesoma hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la menu au namba ya huduma ambayo itarahihisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya fedha. Menu hii mpya inajibu mahitaji hayo yote. 

Ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya, namba mpya ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, SMS na data kila mara watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,’ Umoh alisema.


Alibainisha faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap, zinazowawezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipekee za matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake.

 ‘Tumesoma mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho muafaka linaloendana na mahitaji yao ya kipekee kupitia menu hii inayorahisisha matumizi yao ya simu kupitia mtandao wetu ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini,’ alisema.


Tigo inaendelea kuwa mtandao unaoongoza kwa kuzindua bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Tigo ndio mtandao ulioleta mageuzi makubwa zaidi katika mifumo ya bei ya mitandao ya simu za mkononi nchini. 

Tigo pia ndio iliyokuwa mtandao wa kwanza kuzindua huduma za vifurushi vya sauti na data, ndio mtandao wa kwanza kuzindua simu za kisasa zenye mfumo wa lugha ya Kiswahili na pia ndio mtandao wa kwanza nchini kuzindua huduma ya Tigo Pesa iliyowezesha wateja wake kufanya miamala ya fedha nje ya nchi iliyokuwa na uwezo wa kubadili thamani ya fedha kulingana na thamani ya fedha ya nchi husika.

‘Kupitia Tumekusoma, tunawakaribisha wateja wote wa Tigo wajiunge nasi katika safari hii ya kumbukumbu ya hatua tulizopiga na mafanikio makubwa tuliyopata katika kipindi hiki cha kuwahudumia Watanzania. 

Tunawakaribisha nyote kuungana nasi katika mageuzi ya kidigitali nchini na kufurahia mtandao wetu wa Tigo ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini Tanzania,’ Umoh alisema. 

Menu mpya iliyoboreshwa ya *147*00# inaanza kufanya kazi leo na wateja wa Tigo wanaweza kuanza kupata bonasi murwa kwa manunuzi yote wanayoyafanya. Tunawakaribisha wateja wetu wakae mkao wa kupokea ofa zaidi kabambe huku tukiendelea katika safari hii ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527