Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo (Jumatano).
Waliouawa wametajwa kuwa ni Mtendaji wa kijiji hicho, Shamte Makawa na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.
Habari za awali zinaeleza maiti ya mwenyekiti huyo wa kitongoji bado haijaonekana na nyumba zao zimechomwa moto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amethitisha kutokea kwa mauaji hayo.
Amesema polisi wameenda eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji na ukaguzi.