Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge jijini Dar es salaam ili kupisha uchunguzi dhidi yao.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba amethitisha hilo wakati akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo.
"Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia",alisema.