HUYU NDIYO MBWA MWENYE SURA MBAYA KULIKO DUNIANI


Martha, ametajwa kuwa mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani.

Shindano la kila mwaka ambalo sasa liko katika mwaka wake wa 29 lilifanyika katika eneo la Petalum mjini Carlifornia.

Martha anayemilikiwa na Shirly Zindler aliwashinda wapinzani 13 na kupewa taji na pesa taslimu dola 1,500.

Mbwa huyo mwenye taya kubwa sasa atasafirishwa hadi mjini New York kwa maonyesho ya vyombo vya habari kulingana na waandalizi wa shindano hilo.

Maonyesho hayo ya Sonoma Marin yanasema kuwa shindano hilo huwashirikisha mbwa wengi ambao wameokolewa katika makazi na maeneo ya kukuza mbwa kwa lengo la kuwauza.Mbwa mwenye sura mbaya zaidi duniani

Martha ni mbwa aliyeokolewa ambaye karibia awe kipofu kutokana na kupuuziliwa mbali alisema bi Zindler.

''Baada ya kufanyiwa upasuaji sasa anaweza kuona tena na hahisi uchungu wowote''.

Shirika la habari la AP limesema kuwa Martha aliibuka mshindi kwa kutembea katika ukumbi na kuwavutia majaji.

Majaji hao walimpatia ushindi mbwa huyo kutokana na hisia za watu, sura, tabia na hisia zake.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments