STEPHEN WASSIRA ACHARUKA!!! AGOMEA MATOKEO YALIYOMPA USHINDI ESTHER BULAYA
الخميس, أكتوبر 29, 2015
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, amesema
hakubaliani na matokeo yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo
hilo, Lucy Msoffe, kwa kumpa ushindi wa ubunge Esther Bulaya, wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Mwanza juzi jioni, Wasira alisema matokeo ya
ubunge yalichakachuliwa kutokana na uhesabuji kura kutofuata utaratibu. Wasira
alisema kutokana na hilo, msimamo wake ni kutoyatambua matokeo hayo
yaliyomshangaza na kumwangusha katika mbio hizo za kulitetea jimbo hilo.
Alisema kura katika uchaguzi huo ziliibwa na kilichotangazwa hakitokani na uamuzi wa wapigakura wa jimbo hilo. Wasira alitolea mfano wa kituo kimoja cha kupigia kura, akisema kura 1,000 ziliongezwa kwa lengo la kumsaidia mpinzani wake. Alifafanua
kuwa kituo hicho cha kupigia kura kilionyesha kilikuwa na wapigakura
waliojiandikisha 367, waliopiga kura 276, kura halali zilikuwa 271. Lakini
alisema matokeo katika kituo hicho yalionyesha kuwa chama cha ACT-
Wazalendo kilipata kura moja, CCM kura 120 na Chadema kura 749, na
Msimamizi wa Uchaguzi akatangaza waliojiandikisha walikuwa 1,367. Alisema
hatasaini matokeo hayo kwa sababu ni batili na hawezi kuafikiana nayo
wala kuyatambua huku akisisitiza uchaguzi huo haukufanyika kwa haki.
Hata hivyo, Wasira alisema Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Msoffe
hakutilia maanani barua ya malalamiko aliyoandika kupitia kwa
Mwanasheria wake ili kusitishwa utangazaji wa matokeo hayo. Hata hivyo,
alikanusha tuhuma za kukimbilia jijini Mwanza kwa kile kilichodaiwa ni
kukwepa aibu ya kushindwa, bali alikwenda huko kwa lengo la kupata
ushauri wa nini cha kufanya katika kipindi hiki.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin