Picha_ KONGAMANO KUBWA LA VIJANA ZAIDI YA 130 LAFANYIKA MJINI SHINYANGAHapa ni katika ukumbi wa mikutano wa Vijana Senta Ngokolo mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika kongamano la Vijana zaidi ya 13o kutoka mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na wizara ya Afya na Ustawi kwa kushirikiana na kamati ya uendeshaji huduma za afya mkoa wa Shinyanga.

Kongamano hilo lililenga kujadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo vijana kuhusu suala la afya ya uzazi ikizingatiwa kuwa mkoa wa Shinyanga ni mkoa unaoongoza kwa mimba na ndoa za utotoni.Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Dkt Julius Thomas.

Vijana kutoka shule za msingi na sekondari,vyuoni,mtaani,wazazi,viongozi wa madhehebu ya dini,na wataalam mbalimbali kutoka mkoa wa Shinyanga.

Kongamano hilo pia limehudhuriwa na Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Dkt Elizabeth Kapella.

Malunde1 blog,ilikuwepo eneo la tukio,mwandishi mkuu wa mtandao huu,bwana Kadama Malunde ametuletea picha 38 kutoka eneo la tukio,Fuatilia hapa chini
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Nuru Seni Muya akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema suala la ukatili wa kijinsia,ndoa na mimba za utotoni bado ni changamoto kubwa mkoani Shinyanga


Awali mratibu wa huduma ya afya na uzazi na mtoto kutoka ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Joyce Kandolo amesema mkoa wa Shinyanga katika mikoa ya kanda ya ziwa ndiyo unaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni.

 
Kandoro ameongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa vijana wengi chini ya miaka 19 wanafanya ngono huku vijana wengi wa kike wakibainika kuwa ndiyo wenye maambukizi zaidi ya magonjwa ya ngono na UKIMWI.
 

Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Dkt Julius Thomas akizungumza katika kongamano hilo ambapo kilio cha Wadau wake wakiwemo viongozi wa dini,vijana,wazazi,walimu na wanafunzi walisema asilimia kubwa ya vijana wamekuwa wakipoteza ndoto zao kutokana na kujiingiza katika mahusiano wakiwa na umri mdogo hali inayochangiwa na wazazi kutozungumza na watoto hao juu ya afya ya uzazi.

Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Dkt Elizabeth Kapella akizungumza katika kongamano hilo ambapo alisema jitihada za maksudi zinahitajika ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana katika jamii
Kongamano linaendelea
 
 Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijanakutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Dkt Elizabeth Kapella akisisitiza jambo
Wadau wakiwa ukumbini

kongamano linaendelea

Vijana wakiwa ukumbini

Waandishi wa habari nao walikuwepo

Meza kuu wakiteta jambo


Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Shinyanga Charles Kisangure akichangia mawili matatu katika kongamano hilo la vijana.

Wadau wakiwa ukumbini


Waigizaji kutoka kundi la UMATI Entertainment Group wakiongozwa na mwigizaji maarufu kutoka Bongo Movie Shinyanga Songoro Gadaffi wakitoa burudani katika kongamano hilo la vijana.


Waigizaji kutoka kundi la UMATI Entertainment Group wakiigiza kuhusu changamoto za afya ya uzazi kwa vijana

Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga akizungumza katika kongamano hilo la vijana.


Mwenyekiti wa taasisi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA) tawi la Shinyanga, Bw. Ezra Manjerenga akizungumza katika kongamano hilo la vijana ambapo alisisitiza umuhimu wa vijana kuwa tayari kuzungumzia matatizo yanawakabili ili kuyakabili

Mijadala katika makundi ikaendelea

Wazazi wakiwa ukumbini

Waandishi wa habari nao wakaendelea na mjadala juu ya changamoto za afya ya uzazi kwa vijana

Walimu nao wakaendelea na mjadala

Mijadala ikaendelea....

Vijana wanaendelea na mjadala


Vijana wenye umri wa miaka kati ya 10 hadi 14 wakiwasilisha kazi ya kundi lao juu ya changamoto wanazokabiliana nazo kuhusu afya ya uzazi.


Mwanafunzi wa Chuo cha Muccos Kizumbi bwana Paschal akiwasilisha kazi ya kundi lake

Tunafuatilia kinachoendelea.....


Kijana Mohamed Mustapha kutoka mjini Shinyanga akiwasilisha kazi ya kundi lake
Vijana wakiwa ukumbini


Ustadhi Fadhil Charamanda akizungumza wakati wa kongamano hilo la Vijana.


Mtangazaji wa Radio Faraja bwana Faustine Kasala akiwasilisha kazi iliyofanywa na kundi la waandishi wa habari kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika kuandika habari zinazohusiana na afya ya uzazi kwa vijana.

Kongamano linaendelea...

Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Dkt Elizabeth Kapella akizungumza katika kongamano hilo

Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa Vijana kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Dkt Elizabeth Kapella akizungumza katika kongamano hilo
 Kongamano linaendelea
 
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم