Hii Kali!! CHATU KASHIKWA NA NJAA KALI,AKAAMUA KUMLA NUNGU NUNGU BILA KUJALI MIIBA YAKE,KILICHOFUATIA NI STORI....




Ndani ya hifadhi ya Eland Game Reserve iliyoko KwaZulu-Natal, South Africa mwendesha baskeli alikatisha siku ya June 14 2015, akakutana na chatu mkubwa mzima kabisa aliyeonekana kama amekula na kushiba kupita kiasi… akampiga picha na kushare na watu wake mitandaoni.

Watu wengi walisogea pia nao kujionea tu jinsi chatu huyo alivyo kwa sababu sio kawaida unaweza kukutana na Chatu alafu akakuacha hivihivi… Siku sita baadae yule chatu alikutwa amekufa, wakaja walinzi wa hifadhi hiyo wakampasua ili kujua nini kilichomfanya afe !!



Kumbe chatu alikula nungunungu.. ndani ya tumbo kakutwa nungunungu huyo japo hawana uhakika kama ni kweli nungunungu kasababisha kifo cha chatu huyo.


Unaweza kujiuliza Chatu alianzaje kula Nungunungu na hiyo miba yote !!


Nungunungu alivyotolewa kwenye tumbo la Chatu




Miba ya Nungunungu iliyokutwa ndani ya tumbo la Chatu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527