TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOLEWA ORODHA YA WALIMU WA MASOMO YA SANAA NA BIASHARA WA SHULE SEKONDARI -AJIRA MPYA MWAKA 2014/15
Orodha ya wahitimu wa shahada na stashahada waliopangiwa katika
halmashauri mbalimbali inafanyiwa marekebisho baada ya kubainika kuwa
uongozi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (Sebastian Kolowa University
College-SEKUCO) cha Lushoto uliwasilisha orodha ya wahitimu wapatao 491
wa mwaka 2013 ambao walishaajiriwa badala ya wahitimu wa mwaka 2014.
Kutokana na sababu hiyo, orodha tajwa imesitishwa kwa muda ili kufanyiwa marekebisho na kuwekwa orodha sahihi itakayojumuisha wahitimu wa SEKUCO wa mwaka 2014.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kasoro hiyo.
Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI
Chanzo-EATV