PICHA YA MCHEKESHAJI MAARUFU TANZANIA "JOTI" YAWA GUMZO MTANDAONI

Picha ya mwigizaji mkongwe wa vichekesho “KOMEDI” Lucas Mhuvile ‘Joti’  imewakuna watu wengi  na kufanya kuwa ni moja kati ya picha zinazo” TREND” mtandaoni toka jana. 
Japo kuwa Joti akiwa kama ‘Bi kiboga’ ametokelezea kiofisi zaidi, watu wengi wamejituka wakiangusha komenti nyingi wakielezea kuvunjika kwa mbavu zao kwa kicheko huku wengine wakisema mnuno wake ndio balaa na wengine wakisema skuna ndio sheedah ilimradi kila mmoja kafurahi kwa mtindo wake.
Kiukweli kabisa kijana huyu ni moja kati ya wakali wa KOMEDI pengine sio hapa bongo tu  bali hata Afrika na Dunia .
 “Kwanini lakini!!!!!?????? @jotimdebwedo ..Angalau umefanya siku yangu iwe nzuri kidogo leo... ila sio kwa skuna hizo!!!!  kwa kumuangalia tu anapendezea kufanya kazi wapi!? amefanania na ofisi gani!!???? “- Zamaradi Mtetema aliandika haya mara baada ya kuiona hii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527