MUME AUA MKE WAKE KISHA KUMZIKA KWENYE ZIZI LA NG'OMBE


Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Ubetu Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, amefariki dunia baada ya kupigwa na mume wake sehemu mbalimbali za mwili na kisha kuzika mwili wake kwenye boma la ng'ombe. 


Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema tukio hilo lilitokea Februari 25 mwaka huu saa 11:45 jioni.
 
Akieleza mazingira ya tukio hilo, Kamanda Kamwela, alisema siku ya tukio jirani na familia hiyo alipigiwa simu na mume wa marehemu na kumwambia ameuwa mkewe na kumtelekeza ndani ya bomala ng’ombe.


Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo aliyeuawa ametajwa kuwa ni Jenipher Peter (45). 
 
Alisema alikuwa akiishi na mume wake, Peter Mrosso (43) pamoja na watoto wao watatu. 
 
Alisema mwili wake ulifukiwa ndani ya boma la ng'ombe.

Kamanda alisema taarifa za mauaji ya mwanamke huyo ilitolewa baada ya jirani yake kupigiwa simu na mume wa marehemu, akimtaarifu kuwa amemuua mkewe na maiti ameifukia ndani ya boma la mifugo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527