Makubwa Haya!! MWANAMME HUYU ABADILISHA SURA AFANANE NA MWANAMKE( MADONNA)

madona feki
Watu wanawapenda mastaa, wapo wanaowapenda mpaka wanatamani wafanane nao, mara nyingi tumekutana na hizi story za watu ambao wamekuwa wakifanya majaribio ya kujibadilisha muonekano, maumbile yani ili tu afanane na staa wake anayempenda.


Jordan James alitumia dola 150,000 (zaidi ya mil 270/-)  ili kujibadilisha afanane na Kim Kardashian, safari hii ni Adam Guerra ambaye yeye jitihada zake alikuwa akizifanya ili afanane na Madonna.

Pesa aliyotumia ni paundi 75,000/- (sawa na mil. 210/-) na kutokana na ‘ukarabati’ ambao anataka kuendelea kuufanya kwenye mwili wake mpaka zoezi likamilike kiasi cha pesa kitakuwa kimefikia paundi 100,000/-

Adam anasema anavutiwa sana na Madonna ndiyo maana anafanya kila kitu ili afanane naye.
Madonna
Madonna

“Nimewahi kupanda jukwaani nikamuiga Madonna.. nilipata mashabiki wengi, nimekuwa nikivutiwa naye kwa kila kitu, nimefanya maamuzi yangu binafsi kwa kutumia hela zangu ili nifanane naye kutokana na mapenzi yangu kwake, pia nimepanga kufanya ziara za kimataifa ili kuwadhihirishia watu jinsi gani navutiwa naye“-Guerra

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم