MCHEZAJI NGULI WA SIMBA CHRISTOPHER ALEX MASSAWE AZIKWA HUKO DODOMA

massawe+clipMaelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake wamejitokeza kumzika aliyekuwa mchezaji nguli wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na klabu ya Simba Christopher Alex Masawe aliyefariki dunia Jumapili iliyopita katika hospitali ya Milembe kufuatia kuugua ugonjwa wa kifua kikuu kwa muda mrefu.

Christopha Alex Masawe ambaye moja kati ya matukio atakayokumbukwa na wapenzi wa soka ndani na nje ya nchi ni mkwaju wa mwisho wa penalt ulioyiondosha katika mashindano ya klabu bingwa barani afrika timu Zamalek ya Misri ambayo ilikuwa inashikilia ubingwa wa afrika mwaka 2003.

Mwili wa nguli huyo umezikwa katika makaburi ya Nkuhungu na maelfu ya waombolezaji huku baadhi ya wachezaji waliowahi kucheza nae enzi za soka lake akiwemo mlinda mlango Juma Kaseja na mlinzi Boniphace Pawasa pamoja na wadau wa soka nchini wakazungumzia kile walichokifahamu kuhusu nyota huyu aliyezimika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم