Tumeshuhudia ndoa nyingi zikifungwa siku hizi lakini hazidumu, chache ambazo zimedumu ama zinadumu kwa muda mrefu.
Wanandoa hawa kutoka California,
Marekani ambao walioana miaka 67 liyopita walikufa kwa kupishana saa
chache wakiwa wameshikana mikono.
Floyd Hartwig mwenye miaka 90 na mkewe Violet mwenye miaka 89 wamefariki February 11 mwaka huu wakiwa nyumbani kwao baada ya kuugua kwa muda mrefu.
“Walikua wakifurajia maisha yao kila siku,walipendana sana,walifanya kazi kwa kujituma na kuheshiamiana sana“alisema mmoja wa watoto wao Donna Scharton.
Kutokana na ukaribu wao familia hiyo
baada ya kuwauguza kwa muda mrefu huku wakiwa wamewatengenishia vitanda
baadaye waliamua kuwaweka pamoja.
Floyd
ambaye alikua wa kwanza kufariki baada ya kusumbuliwa na kansa ya
utumbo huku akiwa amemshika mkewe mkono na baada ya saa tano mkewe naye
alifariki na kujikuta wote wakiwa wameshikana mikono pamoja.