KIJANA APANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUMBAKA NA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI


Mkazi wa Tabata, Erasto Clement (22) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na kukana mashitaka ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 16.

Akisomewa maelezo ya awali jana, Wakili wa Serikali Felista Mosha alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan kuwa katika tarehe na mwezi usiofahamika, mwaka jana, Clement pamoja na mlalamikaji walidaiwa kuwa wanafahamiana  kwa muda mrefu.
 
Mosha alidai kuwa Septemba, 2013 mshitakiwa na mlalamikaji walianza mahusiano ya kimapenzi na kumuingilia kimwili mlalamikaji huyo huku akijua kufanya hivyo ni kinyume na sheria.
 
Pia alieleza kuwa mlalamikaji aliripoti taarifa hizo katika kituo cha Polisi na kupewa PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali.
 
Wakili Mosha alidai kuwa mlalamikaji alipofika hospitali alipimwa na kukutwa na ujauzito wa miezi sita.
 
Mshitakiwa alikubali maelezo yake binafsi pia alikana kufikishwa mahakamani hapo kusomewa mashitaka yanayomkabili.
 
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulidai kuwa utakuwa na mashahidi wanne na kielelezo kimoja ambacho ni PF3.
 
Hakimu Hassan aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili Mosi mwaka huu itakapoanza kusikilizwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم