Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 11 | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, December 6, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU "GAMBOSHI" SEHEMU YA 11

  Unknown       Saturday, December 6, 2014


Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya KUMI NA MOJA  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 11

Ilipoishia............
Basi tukaingia mtaani kusaka damu za watu.
Tuliweza kwenda mpaka sehemu ya baharini ambapo tuliona boti moja katikati ya bahari iliyokuwa imebeba watu wapatao 12.

Tulikubaliana kwenda kuiteka hiyo boti ili kuweza kuleta damu zao.
Tuliizingira hiyo boti na kusimama katika pande nne za dunia na mikono yetu kuinyosha kuelekeza kwenye boti pia na nguvu za kichawi zikifanya kazi.

Boti ilianza kuyumba na taratibu boti ilianza kuzama majini pia na sisi tuliwahi kwa ajili ya kuchukua damu zao kabla hawajakata roho.
Tulifika katika boti ilikuwa ndani ya maji, pia tulifika wote katika boti na tulipoigusa ile boti nilishangaa kuona mwanga mweupe kama radi,ukatupiga na wote kwa pamoja tulirushwa juu na kila mmoja aliangukia sehemu yake na mmoja wetu aliweza kupoteza uhai...

Endelea................

Tukiwa tumebakia watatu, na mateka wa boti wakiwa katika harakati za kujiokoa, walifanikiwa kujiokoa lakini boti ilizama. 

Ghafla upepo ulikuja na ulipotupata nguvu za kichawi zilianza upya, kwa vile walikuwa wametawanyika kila mmoja sehemu yake tulikuwa tunawafuata mmoja baada ya mwingine.
Sisi pia tulitawanyika kila mmoja kivyake.

Kwa upande wangu kuna abiria mmoja nilimfuata, nilipomsogelea tu alitamka "KWA JINA LA YESU" .


Akiwa anaogelea juu ya maji, mwili wangu wote ulisisimka na kuhisi kama kichwani kuna mtu anakusanya nywele zangu, alipotamka tena niliishiwa nguvu na kuanguka chini.
Kama kawaida nguvu niliongezewa za kutosha nikanyanyuka, wenzangu walinifuata na kuniuliza vipi ??????? Tunakusubiri wewe tu, damu tumebakiza kiasi kidogo ili kutimiza masharti, na jamaa yule ukifanikiwa tutakuwa tumekamisha zoezi tulilopewa mfUate haraka kabla hajaokolewa!!!!!

Niliwaangalia kwa dharau kwa kuwapandisha na kuwashusha nikamalizia kwa kuwatukana kikwetu "MNYELILE SHI!" nyie mnanituma kama nani????.

Tukiwa tunazidi kubishana sauti ilisikika kwa kusema "mtu huyu akipona mjue maisha yenu yapo hatarini".

 Kila mmoja wetu aliweweseka haraka haraka sote kwa pamoja tukaanza safari ya kumfuta.


Kazi hii nimeifanya zaidi ya miaka minne lakini sikuwahi kupatwa na jaribio kali kama hili, kimoyomoyo nilijisemea.
Sikujua jinsi gani alikuwa anatuona, maana ilikuwa tukifanya tulichokidhamiria kwake alipenda sana kusema neno "KWA JINA LA YESU" kwetu hali ilikuwa mbaya sana tena akirudia zaidi ya mara mmoja mpaka fahamu tulipoteza.

Tulikuja kuzinduka tukiwa sehemu ya kambi, kundi  letu lilikuwa mojawapo ya makundi yaliyofeli mtihani. 

Kiongozi mmoja alikuja sehemu tuliyokaa na kusema "Kuna vijana walishindwa kumuua mtu mmoja, inasemekana huyo mtu ni MCHUNGAJI na anaupako wa kutosha kinachotakiwa yule mtu afe haraka sana kabla siri yetu hajaitoa" kiongozi alipomaliza kuongea aliondoka.


Mimi ndiye niliyeteuliwa kwa ajili ya kumuangamiza na kuhakikisha mchungaji amekufa.

Nilijiuliza maswali mengi sana kwanini wasiende wao? Maana mimi nilishindwa mwanzo!
Kila mchawi aliweza kunichangia nusu ya nguvu za uchawi wake na mmoja wao alinipa nguvu za kijini ili niweze kupambana na MCHUNGAJI.

 Niliahidiwa kuwa nikifanikisha kumuua nitakabidhiwa mtoto wa mfalme wa wachawi anayekaa nchini Nigeria.
Siku ya kuagwa kwenda kazini kumuua MCHUNGAJI, bonge la sherehe lilifanyika ikiwa fulu kula nyama za binadamu na supu za damu za binadamu.

Mfalme aliniita katikati pamoja na binti yake, binti akiwa  amefungwa kitambaa usoni nikapewa nafasi ya kukitoa kitambaa usoni.


Sikuamini machoni mwangu nilipotoa kitambaa mtoto uzuri wake utadhania haendi chooni, tamaa za mwili ziliniingia nilimkumbatia lakini mfalme akazuia akasema wakati bado subirini kwanza.


Niliwaza jinsi ya kumpata na kumuua MCHUNGAJI, nilipata wazo la kujigeuza jinsia na kuwa msichana mrembo. (Jini anauwezo wa kujibadirisha sura yake zaidi ya 70,000) ndio kazi niliyokuwa nayo.

MCHUNGAJI akiwa ndotoni nilimwijia, akiwa katikati ya pori usiku gari yake ilipata pancha na alikuwa hana akiba ya tairi na simu yake ilizima chaji.


Nikiwa safarini kupitia barabara aliyokuwa umepata pancha nilipita karibu yake, na gari yangu akaisimamisha kwa mbele na mimi nilipaki pembeni na kushusha kioo na kumuuliza unasemaje usiku huu? 


Alisema samahani dada kwa jina naitwa MCHUNGAJI Elikana naomba nisaidie gari yangu imepata pancha kama unatairi ya ziada naomba nisaidie.
Nilishuka kwenye gari na kuchukua tairi yangu na spanna, tulisaidiana kuitoa tairi yake na kuweka yangu.

 Tulipomaliza aliniambia "binti nashukuru sana kwa msaada wako mungu atakulipa, naomba twende mpaka kwangu ili nikifika tufungue tairi yako uchukue" 


Nilimjibu asante na tairi chukua kwa jina naitwa Neema, nikaingia kwenye gari yangu na kumuacha anashangaa.
Kwa mara ya pili tena akiwa katika ndoto, aligongwa na gari na miguu yake yote ilivunjika na kila mtu aliyepita karibu yake alikuwa hampi msaada wowote, na yeye alihitaji sana msaada.

 Mimi pia nilikuwa kati ya wapita njia, aliponiona aliniita na kusema "Neema naomba nisaidie" nilimchukua na kumpeleka hospitali.


Hatua niliyokuwa nimeipanga ni kuonana naye uso kwa uso, ilikuwa mishale ya asubuhi nilijiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuonana na MCHUNGAJI.

Nikiwa na mkoba wangu nilienda moja kwa moja kwenye ofisi ya MCHUNGAJI.

Kabla hujafika kwenye ofisi ya MCHUNGAJI lazima upite mapokezi kwanza.


Basi nilimkuta dada mmoja na kumuuliza kama MCHUNGAJI nimemkuta.


Aliniambia yupo na kuniuliza nina ahadi naye? Nilimjibu hapana.


Alichukua simu ya mezani kumpigia MCHUNGAJI, MCHUNGAJI alisema tuende wote ofisini kwake maana mimi nilikuwa mgeni.

Tulipoingia ofisini kwa MCHUNGAJI, MCHUNGAJI alisimama ghafla kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kuita jina Neema!!!!!!! Neema !!!!, 


Dada wa mapokezi aliniuliza unaitwa Neema??? Nilimjibu hapana! Na MCHUNGAJI aliduwaa sana mpaka akaanguka chini akazimia.
Je, nitafanikiwa kumshawishi MCHUNGAJI kufanya mapenzi?????????????

Simulizi hii Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post