MWANAMME ALIYEKUTWA KWENYE DANGURO NA MAKAHABA SASA KUPANDISHWA KIZIMBANI

Mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Alex ambaye hivi karibuni Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilimnasa akiwa kwenye danguro lililopo Sinza Mapambano jijini Dar, anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa kosa la kumjeruhi mmoja wa waandishi wa habari. 

 Taarifa  zinadai kuwa, baada ya jamaa huyo kunaswa kisha kuwafanyia vurugu waandishi waliokuwa wakitimiza majukumu yao na kuwaharibia vitendea kazi vyao, polisi walifika eneo la tukio kisha kumtia mbaroni.

 “Kesi ipo Kituo cha Polisi Mabatini, taratibu za kisheria zinaendelea na wakati wowote atafikishwa mahakamani kwani ameniumiza sana na hali yangu bado si nzuri, kwa hiyo ili iwe fundisho kwa wengine lazima aadabishwe,” alisema mmoja wa waandishi hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم