Updates!! KUHUSU SAKATA LA JAMAA KUMBEMBELEZA MBWA KISHA KUFANYA NAYE MAPENZI NA KUDAIWA KUMPA UJAZITO


LILE sakata la mume aliyetajwa kwa jina la Hamis Juma mkazi wa Majhe Mji Mpya, Ilala jijini Dar kudaiwa na mkewe, Cecilia Hamis kwamba amempa mimba mbwa yameibuka mapya, Uwazi limeyanyaka. 


Ijumaa iliyopita, Uwazi lilifika kwenye ofisi za Taasisi ya Kutetea Haki za Wanyama ambapo mmoja wa maofisa aliyedai si msemaji maalum, alisema wapo katika mchakato wa kufuatilia madai ya mke wa mtuhumiwa huyo kisha kumpandisha mahakamani kujibu mashitaka ya kumdhalilisha mnyama huyo. 
 
Mbwa anayedaiwa kupewa mimba na Bw. Hamis Juma. 

“Sisi ishu yetu si kufuatilia kama kweli amempa mimba bali ni kujiridhisha kama kweli yule mzee ametembea na mbwa hilo linatosha kabisa kumfikisha kortini,” alisema afisa huyo na kuomba jina lake lisichapishwe gazetini.  


WAGOMA MBWA KUUAWA 
Jingine jipya lililotua Uwazi linadai kuwa, baadhi ya majirani wa nyumbani kwa Hamis wamegoma mbwa huyo kuuawa baada ya wengine kutaka kufanya hivyo wakisema hali hiyo itaweza kusababisha mdaiwa huyo kufanya matukio mengine nje ya nyumba yake. 

MENGINE TENA. 
Katika hatua nyingine, Uwazi limebaini kuwa, kumbe mwanaume huyo ana sakata lingine ambapo ana kesi kwenye Mahakama ya Mwanzo Ukonga jijini Dar akikabiliwa na tuhuma za kumfanyia fujo jirani yake. 

Kwa mujibu wa taarifa za kimahakama, ilidaiwa kuwa Hamis alifika nyumbani kwa Alanus Haule ambaye ni jirani yake saa saba usiku wa siku ya tukio akiwa na silaha za kienyeji na chepe akiwa amelewa na kuanza kumtolea maneno ya vitisho huku akijua ni kosa kisheria chini ya kifungu cha sheria 89 (1) B CAP 16.
 
Cecilia Hamis (kulia) akiwa na mume wake (mtuhumiwa) Hamis Juma. 

Kesi hiyo yenye No 873/2014 ambayo inasikilizwa na Hakimu Mwandamizi, Raia Omary kwa mara ya mwisho ilisikilizwa Julai 3, mwaka huu na kuahirishwa hadi Septemba 11, mwaka huu na yuko nje kwa dhamana. 

Habari hii kuhusu Hamis Juma kudaiwa kumpa mimba mbwa, kwa mara ya kwanza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم