MASKINI MTOTO HUYU,AZAMA KWENYE BWAWA LA MAJI HUKO KAHAMA AKIOGELEA,MWILI WAKE WATAFUTWA SIKU NZIMA BILA MAFANIKIO,TAZAMA PICHA NA VIDEO HAPA

Mwili wa marehemu Frank ukitolewa ndani ya bwawa hili baada ya kupatikana-Picha na BICON PRODUCTION-KAHAMA
Mkazi wa mtaa Shunu kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga, aliyejulikana kwa jina la Frank Fred mwenye umri wa miaka 15, amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea kwenye kwenye Bwawa.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni wakati mtoto Frank akiogelea na wenzake katika Bwawa hilo lililopo maeneo ya KTM wilayani Kahama, ambapo alizama kusababisha kifo chake.

Mwili wa Marehemu Frank umefanikiwa kutolewa leo majira ya saa nne asubuhi, ukiwa chini ya kina kirefu katika bwawa hilo, mara baada ya hapo jana wazamiaji mbalimbali kuhangaika kuutafuta bila mafanikio yoyote.


Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga mifugo, alifika katika bwawa hilo akiwa na Panga ambalo inasemekana alitumwa na mwajiri wake kukata majani kwa ajili ya kulisha mifugo hiyo.

Kwa mujibu wa Wachungaji wenzake, Marehemu Frank mara kwa mara amekuwa akiwatizama wenzake wakiogelea huku yeye akiogopa, lakini jana aliamua kuogelea kwa lengo la kujifunza kuogelea kama wenzake na matokeo yake akazama.

Muuguzi mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Richard Mabagala amethibitisha kupokea mwili wa marehemu leo asubuhi, na kwamba umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

Jeshi la polisi wilaya ya kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taratibu za Mazishi zinafanywa na Wazazi wa Marehemu ambao ni wakazi wa Busenda kata ya Kilago wilayani humo.

TAZAMA HAPA VIDEO UONE JINSI MWILI WA MAREHEMU FRANK FRED ULIVYOOPOLEWA MAJINI NA WAZAMIAJI HUKO KAHAMA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments