GEORGE TYSON WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA


George Tyson enzi za uhai wake.



NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma. 

Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya. Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.
Marehemu Tyson akiwa na Monalisa (kushoto), kulia ni Tyson na mwanae Sonia.


 Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Monalisa amemlilia Tyson kwa kuweka picha hiyo juu na kuandika maneno yafuatayo:

 



Taarifa hizi ambazo zimethibitishwa na watu wa karibu yake zinasema kuwa, mauti haya yamemfika baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka walipokuwa wameenda kwa ajili ya kipindi cha The mboni show ambacho yeye alikuwa ndiye muongozaji mkuu.
Wasanii na mastaa mbalimbali nchini wameoneshwa masikitiko yako juu ya kifo hichi ikikumbukwa kuwa ni siku tano tu zimepita tangu mwigizaji Rachel Haule alipotutoka.

Akiwa kazini enzi za uhai wake

Batuli: - Niongee nini, niseme nini Mwenyezi Mungu tusamehe sie waja wako, Yarabbi eeeeeh Mola wng, R.I.P My brother, My shemeji, My director......Eeeeeh Mola mpokee George Tyson wetu, Poleni wasanii wenzangu, Poleni team nzima ya the mboni show thembonishow Pole Monalisa wangu
Rose Ndauka: Ki ukweli sina LA kusema ila asante baba wa mbinguni kwa kila jambo. ...mola mpokee ndugu yetu, kwa mikono salama na umlaze pema peponi ameen.....R.I.P George Tyson.
Agness Masogange: R.I.P George tyson mm siamin bado jmn E Mungu tuhurumie waja wako!
Flaviana Matata : This is very sad aisee,Rest In Peace Tyson.Mungu kakupenda zaidi, - monalisa pole sana dadangu,Mwenyezi Mungu awatie nguvu
Wema Sepetu - Kwa mara ya tatu bila hata kupumzika week... tunamzika mwenzetu mwingine... George Tyson.... Dah... Im just speechless.. RIP brother... Dah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee.... Pole dada akee ... Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya @thembonishow .... Pigo kubwa tena kwa wasanii.... Tunaisha tu jamani.
Aunty Ezekiel - Mungu wang Naomba useme na sisi jaman Mungu baba tuone sisi jaman Naumia siwezi elezea jaman RIP Tyson wang jaman Rip director .....Nakosa lakusema
Mohamed Mwikongi : Hakika yametufika, A film director George Otieno Tyson naye hatunae tena duniani.
George Tyson aliwahi kuwa mume wa mwigizaji Monalisa na kuweza kuzaa naye mtoto mmoja.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527