Duh!! JAMAA ALIYEBAKA MTOTO,ATAKA KUBAKA TENA NDANI YA MAHAKAMA,ALIANZA KWA KUMSHIKA SHIKA MWANAMKE ALIYEKUWA KARIBU NAYE KISHA KUMPIGA MTAMA

Imetokea Kenya ambapo Simon Ngozi (21) alikuwa amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumbaka Mwanamke aliyekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.

Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.

Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke aliyetaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni

Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.

Source: Standard Digital

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم