Breaking News!! RACHEL HAULE "RECHO" WA BONGO MOVIE AFARIKI DUNIA
Tuesday, May 27, 2014
Rachel Haule "Recho" enzi za uhai wake
Habari zilizotifikia hivi punde zinasema kuwa Mwigizaji wa bongo movie Rachel Haule "Recho" amefariki dunia
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam.
Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.
Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana. Kifo hiki kimeleta mshtuko mkubwa kwenye tasnia ya filamu za kibongo.
Habari kamili kuhusu tukio hili tutakuletea hivi punde........... Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Recho.Amina!!
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin