Jamani mtoto huyu!!! AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE SUFURIA YA CHAI JIKONI HUKO MARA

NB-Picha haihusiani na tukio katika habari hapa chini
Mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja amekufa baada ya kutumbukia kwenye sufuria ya chai iliyokuwa jikoni katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Tukio hilo la kusikitisha lililothibitishwa na polisi limetokea juzi majira ya asubuhi katika kijiji cha Kibara B, wilayani humo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kibara B, Bw. Mafwili Munyaga, amesema kuwa mtoto huyo wa jinsia ya kike alitumbukia kwenye sufuria hiyo ya chai iliyokuwa jikoni wakati mama yake mzazi alipomuacha hapo na kuingia ndani ya nyumba.

Bw. Munyaga amesema kuwa baada ya kutumbukia kwenye sufuria hiyo mama yake alisikia kelele za mtoto huyo na kwamba kwa kushirikiana na majirani walimuokoa na kumpeleka katika hospitali ya misheni Kibara, lakini muda mfupi akapoteza maisha.

Kufuatia tukio hilo mwenyekiti huyo amewataka wazazi hasa wanawake kuwa makini na watoto wao kwa kuacha kukaa nao katika mazingira ambayo ni hatarishi kwa maisha yao, ili kujiepusha na majanga yasiyokuwa ya lazima.
 via>> Mara yetu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم