RTO SHINYANGA ASEMA AJALI ZA BARABARANI ZIMEPUNGUA MKOANI SHINYANGA




Imebainishwa  kuwa katika kipindi cha mwezi  Januari hadi mwezi Agosti mwaka huu ajali za barabarani katika mkoa wa shinyanga zimepungua kwa asilimia 12.6  mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo ilikuwa asilimia  33.7

Hayo yamebainishwa juzi na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Shinyanga RTO  Desdery Kamugisha wakati akitoa takwimu hizo kwa waandishi wa habarii, ambapo alisema katika kipindi cha mwezi januari hadi Agosti mwaka zilitokea ajali 167 kati ya ajali hizo zilizosababisha vifo ni  65 ,majeruhi 102 ambapo jumla ya watu waliokufa ni 84  na waliojeruhiwa ni 191.

Aidha alisema ajali nyingi mkoani Shinyanga zinatokana na uzembe wa madereva, ulevi pamoja na waendesha baiskeli maarufu daladala na pikipiki wengi wao wakitokea maeneo ya vijijini wanaofanya shughuli hizo mjini  Shinyanga wengi wakiwa hawajui  sheria na alama za usalama barabarani.

Mwaka jana  katika kipindi kama hicho  zilitokea Ajali 191 kati ya ajali hizo zilizosababisha vifo 98,na ajali zilizo sababisha majeruhi ni 93, na watu waliokufa ni 75, waliojeruhiwa ni 201.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم