Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NG'OMBE AUA MTU HUKO NGOKOLO - SHINYANGA MJINI


Ng'ombe aliyesababisha kifo.
***

Mzee Monisa, mfugaji na Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na ng’ombe katika tukio lililotokea Alhamisi, Septemba 3, 2026, majira ya saa 3:00 asubuhi.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea baada ya watu kufika kumchukua ng’ombe huyo kwa ajili ya kwenda kumpandisha jike. 

Inadaiwa kuwa walipomfikia, ng’ombe huyo alikimbia na kufika katika eneo la jirani, anakoishi Mzee Monisa.

Mzee Monisa alichukua fimbo na kujaribu kumrudisha ng’ombe huyo, lakini ng’ombe huyo alimgeukia na kumkanyaga.

Baada ya tukio hilo, Mzee Monisa alikimbizwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya matibabu.

 Inadaiwa kuwa baada ya kufanyiwa vipimo, ilibainika kuwa alikuwa amevunjika mbavu, lakini alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Mzee Monisa alikuwa mfugaji, na hadi umauti ulipomkuta alikuwa akihudumu kama Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Ngokolo.

Pia, Mzee Monisa aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwinamila, Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Peponi. Apumzike kwa amani. 🙏🏾💔

Tutawaletea taarifa kamili hivi punde.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com