Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZZA AWAHAKIKISHIA WANANCHI WA NSALALA UPATIKANAJI WA MAJISAFI NA SALAMA

 



Nar Marco Maduhu, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amewahakikishia wananchi wa kijiji cha Nsalala wilayani Shinyanga juu ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama.

TAZAMA VIDEO👇👇

Amebainisha hayo leo Septemba 28,2026 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wa hadhara, ambapo kero yao kubwa ni kilio cha upatikanaji wa maji safi na salama.

Amesema, ajenga ya maji ni ya jimbo zima la Itwangi, na kwamba amekuwa wakilisemea Bungeni, na kwamba wakati wakiendelea kusubili Maji ya Ziwa Victoria kufika katika kijiji hicho cha Nsalala, aliona ni vyema visima vya maji vya awali ambavyo viliharibika visafishwe na mashine na kuhudumia wananchi.

“Kisima kimoja kilichimbwa enzi za utawala wa marehemu Mzee Mwinyi na visima vyote vilili kimoja kilikuwa kinapeleka maji Nsalala na kingine Mwamkanga, nilisema haiwezekani ni kaa kusubiri mradi wa maji ya Ziwa Victoria na wakati tunavisima hapa,” amesema Azza.
Ameongeza kuwa, aliongea na Waziri wa Maji na Katibu Mkuu Wizara ya Maji wakatuma mashine ambazo zikafungua visima hivyo na vikakutwa visafi na maji yapo ya kutosha ambapo kisima cha kwanza kwa majibu ya wataalamu kinauwezo wa kutoa maji Lita 15,000 kwa saa moja na kingine Lita 10,000 kwa saa moja.

“Maji haya tuliyaonja hayana chumvi hata kidogo,” amesema Azza.

Ameongeza kuwa, baada ya Wataalamu kurudisha majibu kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji , alitoa ahadi kuwa haita fika Mwezi wa 12 Mwaka huu, wataleta pampu na kurudishia miundombinu ya mabomba na kuweka vituo vya kuchotea maji, wakati wakisubiri mradi wa Maji ya Ziwa Victoria.
Amezumgumzia pia barabara ya Nsalala- Butindi kwamba daraja lake lilivunjika muda mrefu, na kwamba ukifika Nela mvua za mwaka jana zilivunja karavati na pakawa hakuna mawasiliano, lakini Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ,kutokana na kwamba hataki wananchi wake wapate shida, ametoa fedha za ujenzi wa daraja hilo pamoja na karavati.

Katika hatua nyingine amezungumzia skimu ya umwagiliaji ya Nsalala na Skimu zingine kwamba ameshazisemea bungeni na kwamba serikali itakuja kutengeza mirefeji hiyo .
Aidha, amewapongeza pia wananchi wa kijiji hicho cha Nsalala kwa kuanzisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho, na kuamua kuwaunga mkono kwa kutoa sh.Milioni Moja "Cash".

Kwa upande wake Meneja huduma kwa wateja SHUWASA, Masaka Kambesha, amesema Mamlala hiyo hua inamipango ya muda mrefu na mfupi na kwamba ya muda mfupi ndiyo hiyo ya ujenzi wa visima vya maji, na kwamba walifika Nsalala na kufanya usanifu na kuona uwezo na maji ya visima hivyo na kufika Desemba huduma ya kufufua visima hivyo itakuwa imeanza.
Amesema mpango wa muda mrefu ni kusambaza Maji ya Ziwa Victoria, na walishafanya usanifu na sasa wapo kwenye hatua nzuri ya kusambaza maji hayo katika vijiji kikiwamo cha Nsalala na sasa wanasubiri kupitishwa kwa andiko.

Nao baadhi ya wananchi wamempongeza Mbunge Azza kwa kuendelea kutatua changamoto ambazo zinawakabili wananchi hasa tatizo la maji.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nsalala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com