Mbunge wa Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, ameendelea kuonesha ushirikiano wake na sekta ya kilimo kwa kukutana na viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku, vyama vya ushirika, taasisi za fedha pamoja na wadau mbalimbali wanaohusika na uzalishaji na biashara ya zao la tumbaku katika Halmashauri ya Ushetu, mkoani Shinyanga.
Kikao hicho kimefanyika leo, Septemba 15, 2026, katika Ukumbi wa Shule ya Amali, Kata ya Nyamilangano, Halmashauri ya Ushetu.
Kikao hicho kililenga kujadili kwa kina changamoto zinazowakabili wakulima wa tumbaku na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua, ili kuhakikisha wakulima wanapata tija kutokana na juhudi na gharama wanazotumia katika uzalishaji wa zao hilo, ambalo ni miongoni mwa mazao muhimu ya biashara katika eneo la Ushetu.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho, Mhe. Cherehani amesema ameamua kuwakutanisha wadau hao kwa sababu kilimo ni mhimili muhimu wa uchumi wa wananchi wa Ushetu, hivyo ni muhimu changamoto zinazowakabili wakulima zisikilizwe na kutafutiwa ufumbuzi kwa kushirikisha wadau wote wenye nafasi katika mnyororo wa thamani wa zao la tumbaku.
Amesema moja ya hoja zilizojadiliwa ni ucheleweshwaji wa malipo kwa wakulima baada ya kuuza tumbaku yao, akieleza kuwa suala hilo linahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, amewataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wanaodaiwa kuwadhulumu wakulima kwa kutowalipa fedha zao kwa wakati, akiwataka kuacha tabia hiyo na kuhakikisha madeni yote ya wakulima yanalipwa kwa wakati.
Cherehani ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kilichowakutanisha viongozi wa AMCOS na wadau wa zao la tumbaku katika Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ambapo amesisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuwa waadilifu na kutanguliza maslahi ya wakulima wanaowahudumia.
Amesema viongozi ambao bado hawajalipa fedha za wakulima wanapaswa kufanya hivyo mara moja, kabla hatua za kisheria hazijaanza kuchukuliwa dhidi yao.
Aidha, kikao hicho kimezitaka kampuni ambazo bado zina madeni kwa wakulima wa tumbaku kuhakikisha zinakamilisha malipo hayo kabla ya tarehe 30 Septemba.
Kwa upande wake, Happiness Mpena, kwa niaba ya Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, amewataka viongozi waliopewa dhamana kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa uadilifu, akieleza kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), ameahidi kutekeleza maagizo na ushauri uliotolewa katika kikao hicho.
Social Plugin