Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TTCL PESA YARAHISISHA MALIPO KWA WAKULIMA, WAFANYABIASHARA NCHINI



Na Sheila Ahmadi, Dodoma

TTCL Pesa imewahimiza vyama vya ushirika kutumia huduma ya Malipo kwa Mkupuo inayowezesha wakulima kulipwa moja kwa moja kupitia simu zao, bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia.

Akizungumza kwenye Maonyesho ya nanenane jijini Dodoma kuhusu huduma hiyo, Afisa Mauzo kutoka TTCL Pesa, Osna Boaz, amesema mfumo huo umeundwa kurahisisha malipo kwa vyama vya ushirika vinavyohitaji kuwalipa wakulima wengi kwa wakati mmoja.

Amesema badala ya chama kufanya malipo kwa mkulima mmoja mmoja, mfumo huo unaruhusu kupakia orodha ya wanufaika wengi, ambapo taarifa zao huchakatwa na malipo kufanyika kwa wakati mmoja.

“Huduma hii inarahisisha mfumo mzima wa malipo na kupunguza mlolongo wa vyama au viongozi kutembea na fedha wakati wa kuwafikishia wakulima malipo yao,” amesema "Boaz

Aidha, Boaz amewaalika wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutumia huduma ya Lipa Namba, ambayo inawawezesha kupokea malipo kutoka kwa wateja wanaotumia mitandao mbalimbali ya simu.

Katika hatua nuingine huduma hiyo inapatikana pia kwa wafanyabiashara wadogo wenye majina binafsi, ambapo wanahitaji kuwa na kitambulisho ili kupatiwa Lipa Namba inayoweza kupokea malipo kutoka mitandao yote.

Vilevile Boaz, matumizi ya malipo ya kidijitali yanaendelea kuwa muhimu katika kuongeza usalama wa fedha na kurahisisha miamala kwa wafanyabiashara na wananchi.

mfanyabiashara anayekuwa na huduma ya Lipa Namba anaweza kuendelea kuwahudumia wateja ambao hawana fedha taslimu, hivyo kupunguza uwezekano wa kupoteza wateja.

Nitoe wito kwa wafanyabiashara na vyama vya ushirika kujitokeza na kutumia huduma hizo, akisisitiza kuwa mfumo wa Malipo kwa Mkupuo ni rahisi na unawezesha vyama kufanya malipo kwa wanufaika wengi kwa wakati mmoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com