Na Sheila Ahmadi, Dodoma
Kampuni ya Simba Tanzania Limited imewahimiza wananchi kutumia fursa zilizopo katika sekta ya ufugaji wa kuku kwa kuanzisha na kuendeleza miradi ya ufugaji yenye tija, huku ikitoa elimu kuhusu upatikanaji wa vifaranga na chakula cha kuku.
Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Dodoma, Meneja Mauzo kutoka kanda ya kati Ditirick Mdemu amesema kampuni ya Silverlands inajihusisha na uzalishaji wa vifaranga pamoja na chakula cha kuku huku ikilenga kuwawezesha wafugaji kupata mahitaji muhimu kwa ajili ya uzalishaji.
Sanjari na hayo kampuni hiyo inatoa aina mbalimbali za vifaranga, ikiwemo vifaranga vya kuku wa nyama, kuku wa mayai pamoja na aina nyingine zinazofaa kwa wafugaji wenye mahitaji tofauti.
kwa sasa wananchi wengi wameanza kuangalia ufugaji wa kuku kama fursa ya biashara, hali inayoongeza uhitaji wa taarifa sahihi kuhusu ufugaji, lishe, magonjwa na namna bora ya kuendesha miradi hiyo.
“Watu sasa hivi wanataka biashara. Wafugaji wanauliza maswali mengi kuhusu chakula, magonjwa na namna ya kuendesha mradi wa ufugaji,” amesema Mdemu".
hali hiyo inaonesha kuongezeka kwa mwamko wa wananchi katika kuwekeza kwenye ufugaji wa kuku, hivyo kampuni inaendelea kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji ili waweze kufanya shughuli hiyo kwa ufanisi.
Aidha, niwakaribishe wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane kufika katika banda la kampuni hiyo kwa ajili ya kupata elimu zaidi kuhusu vifaranga, chakula cha kuku na masuala mbalimbali yanayohusu ufugaji.
Vilevile wananchi wanaweza kupata taarifa zaidi kuhusu huduma na bidhaa za kampuni hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Social Plugin