OFISI YA TAKWIMU YAELEZA MAFANIKIO YA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA,YATAJA VIFO VYA UZAZI KUPUNGUA

 


Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 blog,Dodoma.

OFISI ya taifa ya Takwimu imeeleza kuwa vifo vitokanavyo  na uzazi vimepungua kwa kasi kubwa kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100000 kwa Mwaka 2015/2016 hadi kufikia vifo 104 kwa vizazi hai 100000 kwa Mwaka 2021/2022 sababu ikitajwa kuwa ni kutokana na bajeti ya wizara ya afya kupewa kipaumbele 

Hayo yamesemwa leo March 22,2024 Jijini hapa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa wa Takwimu Dkt Albina Chuwa wakati akitoa taarifa kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita  katika kipindi cha miaka mitatu. 

"Katika kipindi cha miaka mitatu tafiti mbalimbali za kijamii kiuchumi na mazingira zimefanyika zikiwemo, Utafiti wa afya ya  uzazi na mtoto na viashiria vya malaria wa Mwaka 2022 ambapo ulionesha kuwa  sekta ya afya imeendelea kuimarika katima maeneo yote, " amesema

Amesema vifo vinavyotokana na uzazi  na watoto chini ya miaka mitano na kuendelea ndivyo vimeweka rekodi na kuiletea sifa nchi ya Tanzania  kimataifa. 

"Lengo ni kufikia Mwaka 2030 wakati wa kuhitimisha agenda 2030 ya SDGs kusiwepo na vifo vitonavyo na uzazi, " amesema. 

Kwa upande wa maambukizi ya UKIMWI amesema utafiti uliofanyika matokeo yameonesha kuwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea wanaoishi na na VVU vineendelea kupunga kutoka asilimia 4.9 Mwaka 2016/17 hadi asilimia 4.4 Mwaka 2022 hadi 2023.

"Maana yake ni kwamba Serikali ya awamu ya sita imeendelea na juhudi zake zakupambana na maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI kwa Wananchi wake na hususan vijana na vijana wa like kwa kuwawezesha zaidi kujipatia kipato Chao cha mahitahi ya Msingi kila siku, " Amesema Dkt Albina. 

Katika utafiti wa kutathimini upatikanaji wa huduma za maji ambapo Takwimu rasmi za mafanikio katika Sera ya maji na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya sita " Kumtua Mwanamke Ndoo Kichwani"

Amesema Matokeo ya Sensa ya watu na ma kazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa wana wake walio wengi wanaongoza kaya kwa sasa  kutoka asilimia 33 ya Kaya zone nchini Mwaka 2012 hadi asilimia 36 mwaka 2022.

" Mafanikio haya ni makubwa kwa Mwanamke kutambulika katika jamii ya kitanzania ya kuwa Mkuu wa kaya kwa kutoa maamuzi ndani ya kaya na katika vyombo vya maamuzi katika Serikali ya awamu ya sita wanawake wamepewa nafasi, "amesema

Amesema Ofisi ya  Takwimu itaendelea  kuona kuwa kaya zinazoongozwa na wanawake matokeo ya Sensa yanaonesha kuwa kwa wastani, asilimia 71.4 ya kaya hizo zinatumia maji kwenye vyanzo vilivyoboreshwa kwa mujibu wa lengo la sita la SDGs.

Pamoja na mambo mengine amegusia hali ya uchumi mwa mwananchi wa kawaida kulalamikiwa kuwa ni mgumu kwa kueleza kuwa watanzania wanapaswa kufanya kazi na kwamba duniani kote hakuna Serikali ambayo imewahi kugawa fedha kwa mwananchi mmoja mmoja. 

"Ni kweli maisha magumu lakini njia pekee ya kijinasua ni kufanya kazi kwa bidii kupitia fursa ambazo Serikali inawapatia, ugumu wa maisha umetokana na sababu za Vita vya Urusi na Ukrain pamoja ugonjwa wa UVICO, " amesisitiza Dk. Chuwa. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم