EWURA YASHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE LA KUGAWA MITAJI NA VITENDEA KAZI VYA NISHATI SAFI YA KUPIKIA








MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza katika banda la Mamlaka hiyo leo Machi 9,2024 jijini Dodoma kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.

Na Alex Sonna-DODOMA

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,amesema mamlaka hiyo ina wajibu kuhakikisha wanamtua Mwanamke kuni na Mkaa kichwani kwa kuhakikisha wanatoa leseni kwa wakati kwa wawekezaji wanaokuja nchini kuwekeza katika nishati safi ya kupikia.

Dkt. Andilile ameyasema hayo leo Machi 9,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.


Amesema taifa bado linatumia nishati isiyosafi kwa kupikia hivyo EWURA itahakikisha ina wajibu wa kuhakikisha inatekeleza mikataba ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza ikiwemo uharibifu wa mazingira na madhara ya afya yanayosababidhwa na moshi wakati wa matumizi ya kuni na mkaa.

“EWURA tutahakikiha tunahamasisha uwekezaji katika nishati safi kwa kutoa leseni kwa wawekezaji kwa wakati ili wawekeze katika eneo hilo, pia tunaangalia upatikanaji wake katika maeneo mengi kwa kuangalia mwenendo wa bei za bidhaa hiyo,” amesema Dkt. Andilile.

Ameongeza kuwa:”Sisi kama EWURA tutahakikisha kama ilivyo dhamira ya Rais kumtua ndoo mama kichwani, tutamtua mwanamke kuni kichwani kwa kuhakikisha anatumia nishati ambayo itamrahisishia kupata maendeleo badala ya kuhangaika na nishati chafu ya kupikia,”.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Machi 9,2024 jijini Dodoma katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.


MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Machi 9,2024 jijini Dodoma katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza katika banda la Mamlaka hiyo leo Machi 9,2024 jijini Dodoma kwenye Kongamano la wanawake la kugawa mitaji na vitendea kazi vya nishati safi ya kupikia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم