RC MNDEME AKABIDHI MIPIRA 1000 KUTOKA TFF KUIBUA VIPAJI VYA WANAFUNZI SHINYANGA

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amekabidhi mipira ya miguu 1000 kwa Maafisa Michezo katika Halmashauri Sita za Mkoa huo, kwa ajili ya kuibua vipaji vya wanafunzi kwa shule za Msingi.
Makabidhiano ya Mipira hiyo yamefanyika leo Februari 28,2024 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Mipira iliyotolewa na Shirikisho la Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Mndeme akizungumza wakati wa Makabidhiano ya Mipira hiyo, ameipongeza TFF kwa kuhamasisha Michezo mashuleni kwa lengo la kuibua vipaji vya wanafunzi.
"Tunaipongeza TFF kwa kutupatia Mipira 1000 kwa ajili ya kuhamasisha Michezo kwa wanafunzi wa shule za Msingi,ili kuibua vipaji vya watoto wetu," amesema Mndeme.

Amewataka Walimu wa Michezo wahakikishe Mipira ambayo wamepewa wasiiweke Stoo, bali ikatumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa, ikiwa ni sehemu pia ya kujiandaa na Michezo ya UMITASHUMITA na UMISETA.
Aidha, amesema pia Serikali kupitia kila Halmashauri,wametenga fedha kwa ajili ya kuboresha Sekta ya michezo na matarajio ya Mkoa ni kuona vijana kutoka Shinyanga wakicheza AFCON.

Pia amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maboresho makubwa ambayo ameyafanya katika Sekta ya Michezo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mipira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Said Mankiligo, amesema Mipira hiyo imetolewa kwa Mikoa 12 ya Tanzania Bara na Miwili Zanzibar, lengo ni ni kuibua vipaji vya michezo kwa wanafunzi.

Amesema Mipira hiyo kwa upande wa Manispaa ya Kahama, wanapewa Mipira 200, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mipira 200, Ushetu 150,Msalala 150, Kishapu 150 na Shinyanga Manispaa mipira 150.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) Said Mankiligo (kulia) akimkabidhi Mpira Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme kati ya Mipira 1000 ambayo imetolewa na TFF kwa ajili ya Michezo kwa wanafunzi wa Shule za Msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akikabidhi Mipira kwa Maafisa Michezo wa Halmashauri za Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akikabidhi Mipira kwa Maafisa Michezo wa Halmashauri za Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kulia) akikabidhi Mipira kwa Maafisa Michezo wa Halmashauri za Mkoa huo
Muonekano wa baadhi ya Mipira kati ya Mipira 1000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم