WASHINDI WA ‘TWENDE AFCON’ NA BETWAY ‘WAPAA’ KWENDA IVORY COAST

MKAZI wa Dodoma Prisca S amepaa kwenda Ivory Coast kushuhudia mashindano ya Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) ikiwa ni awamu ya pili ya washindi wa Promosheni ya ‘Twende AFCON’ inayoendeshwa na kampuni ya Betway Tanzania.

Promosheni hiyo iliyozinduliwa Novemba Mwaka jana, pamoja na mambo mengine ilikuwa na lengo la kuwapatia fursa watanzania hususani watumiaji wa mtandao wa kubashiri wa Betway kwenda kuiunga mkono Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) iliyokuwa ikishiriki pia mashindano hayo.

Akizungumzia fursa hiyo Prisca amesema kwake imekuwa ni furaha kubwa kwenda kushuhudia michuano hiyo yenye thamani kubwa Barani Afrika akiamini kuwa itamsaidia kumuongezea uelewa Zaidi katika masuala ya soka la Afrika na ushindani uliopo baina ya nchi na nchi huku ikimpa fursa ya kukutana na watu mbalimbali.

“Namshukuru Mungu kupata nafasi hii, kwangu ni mara ya kwanza kusafiri kwenda Ivory Coast, pia fursa ya kuiona michuano hii mikubwa mubashara nikiwa uwanjani wakati mchezo ukiendelea” amesema Prisca huku akishukuru Betway Tanzania kwa kuleta Promosheni hiyo iliyompatia fursa hiyo

Kwa upande wake Balozi wa Betway Tanzania Salama Jabir amesema Promosheni iliyo iliyodumu kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Novemba 16 hadi Desemba 16, ilikuwa na lengo la kuwapa fursa watanzania kwenda nchini Ivory Coast kuishuhudia michuano hiyo lakini pia kuipa sapoti timu ya Taifa ya Tanzania ambayo tayari ilishayaaga mashindano hayo.

“Tunajua timu yetu ilikuwa Ivory Coast kushiriki michuano ya AFCON, kwa hiyo Promosheni yetu ilienda na mkakati wa kuwawezesha watanzania kwenda kuipa nguvu, lakini kwa bahati mbaya wapiganaji wetu waliondolewa; tunaamini wakati ujao itafanya vizuri zaidi na zaidi kwani hata mwaka huu imeonyesha nguvu kubwa”, amesema Salama.

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 ambayo kwa sasa inaingia hatua ya nusu fainali ilianza nchini humo Januari 13 na kutarajiwa kuhitimishwa Februari 11 ilizijumuisha timu kutoka Mataifa 24 ikiwemo Tanzania ambayo kwa Mwaka huu imeshiriki kwa mara ya tatu tangu ilipofuzu kwa mara ya kwanza 1980,2019 na mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments