ZIMAMOTO YAWAZIMA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA

 

Shamrashamra za kusherehekea ushindi wa Mbuzi zikiendelea.


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, wameibuka kidedea Bonanza la Michezo wa mpira wa miguu kati ya Waandishi wa Habari mkoani humo, baada ya kuwafunga kwa Mikwaju ya Penati na kisha kuondoka na Mbuzi.
Bonanza hilo la Michezo limefanyika leo Februari 23, 2024 katika Viwanja vya Jeshi la Zimamoto maeneo ya Soko la Nguzonane Manispaa ya Shinyanga.

Michezo huo wa Mpira wa Miguu, ambapo dakika 90 ulimazika kwa kufungana kwa goli Mbili kwa mbili, na kisha kwenda kwenye Mikwaju ya Penalti na Jeshi la Zimamoto lilifunga Mikwaju Penati 4-3 na kuondoka na Mbuzi.
Aidha, katika Bonanza hilo imefanyika pia michezo mbalimbali ikiwemo ya kufukuza kuku, ambapo washindi waliondoka na kuku, pamoja na kukimbiza Magunia na kuruka Sarakasi.

TAZAMA PICHA ZA BONANZA LA MICHEZO 👇👇
Mechi ikichezwa kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Waandishi wa habari wenye Jezi za Njano.
Kabumbu likiendelea kusakatwa.
Mechi ikiendelea kuchezwa.
Mikwaju ya Penati ikipigwa.
Mikwaju ya Penati ikiendelea kupigwa.
Wakuu wa Jeshi la Zimamoto Mkoa na wilaya ya Shinyanga wakishuhudia Mtanange wa Mchezo huo.
Mshabiki wakiwa uwanjani.
Mashabiki wakiendelea kushuhudia Mechi Kati ya Askari wa Zimamoto na Waandishi wa Habari.
Mashabiki wakiendelea kushuhudia Mechi hiyo.
Mashabiki wakiendelea kushuhudia Mechi hiyo.
Mashabiki wakiendelea kushuhudia Mechi hiyo.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Martin Nyambala (kulia) akikabidhi Mbuzi kwa washindi wa mchezo huo, ambao ni Askari kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Shamrashamra za kusherehekea ushindi wa Mbuzi zikiendelea.

Chanzo _ Shinyanga Press Club blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم